Kuhusu Sisi

Geita Gold football Club ni timu iliyoanzishwa Mwaka 2009 ikifahamika kama Geita Veterans ikiwa chini wa viongozi kadhaa wa mpira na umoja wa wachezaji wa mpira wa miguu wa zamani ,Mwaka 2011 ikaanza mashindano ya ligi daraja la tatu (3) ikifahamika hivyo kama Geita Veterans ,Mwaka 2012 ikapata nafasi ya kucheza ligi daraja la Pili. 2013 Jina Geita Gold Veterans likabadilika na timu ikaitwa Geita Gold Sports Klabu hapo ndio ilipoanza kushindana kwa ngazi za Juu. Baada ya kuanza kufanya vizuri zaidi mwaka 2016 timu ikabadili jina na ikaitwa Geita Gold Football Club .

Geita Gold Football Club ipo chini ya Halmashauri ya Mji wa Geita chini ya Mkurugenzi wa Halmashauri na Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya Mji Geita. Geita Gold Football Club 2014-2019 timu imecheza ligi daraja la kwanza kwa sasa (Championship ) na haikufanikiwa kupanda kwa msimu huo lakini Msimu wa 2018/2019 timu ilimaliza nafasi ya 3 na ikacheza "Play Off " ya kuwania kupanda daraja dhidi ya Mwadui na haikufanikiwa . Msimu wa 2019/2020 timu ilimaliza nafasi ya 3 na ikacheza "Play Off" tena kuwania kufuzu ligi kuu ya soka dhidi ya Mbeya City na haikufanikiwa .

2020/2021 timu ya ikafanikiwa kupanda daraja kutoka daraja la kwanza "Championship" kwenda ligi kuu soka Tanzania bara "Premier League (TPL). 2021/2022 Geita Gold Footbal Clab imeanza rasmi kushiriki Ligi kuu soka Tanzania bara (TPL) na inafanya vizuri kwa sasa ikiwa katika nafasi za juu za msimamo wa ligi kuu ya soka Tanzania bara. Geita Gold Football Club imeanzisha timu ya vijana walio na umri usiozidi miaka 20 kwa lengo la kukuza talanta za wachezaji na kukuza muamko wa mpira wa miguu Tanzania. Geita Gold kwa sasa inadhaminiwa na Mdhamini Mkuu kampuni ya uchimbaji wa madini Geita "Anglo Gold Ashant Tanzania". Pamoja na wadhamini wengine wanaojitokeza kufanya biashara na klabu hii

TAKWIMU

Zetu

0
Jumla ya mechi tulizocheza
0
+
Jumla ya mechi tulizoshinda
0
Jumla ya mechi tulizotoka sale
0
Jumla ya mechi tulizopoteza
0
Jumla ya alama tulizovuna
Translate ยป